Girl in a jacket

MINISTRY OF HEALTH

National Malaria Control Programme (NMCP)

Girl in a jacket

KATIBU TAWALA WA MKOA WA KIGOMA AZINDUA KAMPENI YA UGAWAJI WA VYANDARUA VYENYE DAWA MKOANI HUMO

Posted on: March 11th, 2025

Katibu tawala wa mkoa wa Kigoma Bw. Hassan Rugwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa huo Mhe: Thobias Emiry Andengenye  amezindua kampeni ya ugawaji wa vyandarua vyenye dawa vinavyotolewa na Serikali ya Tanzania bila malipo kwa wananchi mkoani Kigoma. Uzinduzi huo umefanyika tarehe 11 Aprili 2025.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Katibu Tawala huyo amesema kuwa kampeni hii ya ugawaji wa vyandarua katika mkoa wa Kigoma ni jitihada za mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Dkt Samia Suluhu Hassan katika kupambana na magonjwa mbalimbali yanayaosumbua afya na ustawi wa jamii ukiwemo ugonjwa wa malaria

“Kama mnakumbuka vizuri miaka ya nyuma, Mkoa wetu umewahi kuongoza kwa kuwa na maambukizi makubwa ya ugonjwa wa malaria kitaifa, lakini jitihada za Serikali yetu pamoja na wadau mbalimbali walipambana kwa kuleta afua mbalimbali ikiwemo ya unyunyuziaji wa dawa ya ukoko majumbani  hadi kupelekea kushuka kwa  maambukizi na vifo vilivyotokana na ugonjwa huo”

 Katibu Tawala huyo ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Kigoma kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi ya idadi ya watu katika kaya zao wakati wa zoezi la uandikishaji litakapoanza ili kila kaya wapate vyandarua kulingana na idadi ya watu waliopo wakati wa ugawaji utakapofika. Vilevile amewasisitiza watendaji ndani ya Mkoa wake kutoa ushirikiano kwa wataalam wa Wizara ili kuhakikisha kampeni hiyo inatekelezwa kwa ufanisi mkubwa ndani ya Mkoa wa Kigoma.

Kwa upande wake Bwana Winfred Mwafongo akiongea kwa niaba ya Meneja wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria amesema kuwa wanategemea kugawa vyandarua takribani 1,414,251 kwa Mkoa mzima wa Kigoma na zoezi hilo litatanguliwa na kufanya vikao vya uhamasishaji ngazi za wilaya sasa likifuatiwa na kutoa mafunzo ya uandikishaji kwa waandikishaji watakao pita kila kaya kuchukua taarifa sahihi za idadi ya watu kwenye kaya katika Halmashauri zote 8 za mkoa wa Kigoma

}