Girl in a jacket

MINISTRY OF HEALTH

National Malaria Control Programme (NMCP)

Girl in a jacket

KIKAO CHA KIKOSI KAZI CHA WATAALAMU WA UCHUNGUZI NA MATIBABU YA MALARIA KINAFANYIKA MKOANI DAR ES SALAAM

Posted on: February 4th, 2026

Kikao cha Kikosi kazi cha Wataalam wa Uchunguzi na matibabu ya ugonjwa wa Malaria kinafanyika leo tarehe 3 hadi 4 Januari 2026, mkoani Dar es salaam.
Akifungua kikao hicho, Mkuu wa Kitengo cha Uchunguzi na Tiba ya Malaria Kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Dkt. Abdallah Lusasi, ameleeza kuwa lengo la Kikao hicho ni kujadili masuala mbalimbali ya kitaalamu yanayohusu afua za uchunguzi na tiba ya malaria ikiwemo kuwasilisha hatua za utekelezaji zilizofikiwa katika kutekeleza afua hizo, matokeo chanya yaliyopatikana, changamoto zilizopo na kujadili namna bora ya kuzitatua changamoto hizo.

Afua za uchunguzi na tiba zinazojadiliwa ni pamoja na uchunguzi wa vimelea vya malaria, tiba sahihi ya malaria, Tiba Kinga ya Malaria kwa wajawazito, afua ya vipimo na matibabu ya malaria ngazi ya jamii, hususani kwenye maeneo yasiyofikika kwa urahisi, Tiba Kinga ya malaria kwa wanafunzi shule za msingi na usugu wa vimelea dhidi ya dawa za kutibu malaria.

Aidha, kikao hicho kinachojumuisha wataalamu kutoka maeneo mbalimbali ya kiutaalam, ikiwemo Wizara ya Afya, Taasisi za utafiti, Wadau wa maendeleo, wadau watekelezaji, Asasi za Kijamiii na Washauri elekezi, kitajadili pia maeneo ya vipaumbele katika Mpango Mkakati mpya wa Malaria wa mwaka 2026-2030 na kinatarajiwa kutoka na maazimio muhimu ambayo yatasaidia katika kutoa mwongozo wa sasa na wa baadae katika kuboresha afua hii ya uchunguzi na matibabu ya malaria ili huduma za malaria ziendelee kutolewa kwa ubora na kwa manufaa ya wananchi wote.

}