Girl in a jacket

MINISTRY OF HEALTH

National Malaria Control Programme (NMCP)

Girl in a jacket

KIKAO KAZI CHA KUHUISHA MWONGOZO WA UFUATILIAJI WAGONJWA WA MALARIA CHAFANYIKA MOROGORO

Posted on: November 2nd, 2026


Wizara ya Afya, kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP), imeanza kuboresha na kuhuisha mwongozo wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa afua za Kudhibiti Malaria.

hicho kinafanyika mkoani Morogoro na kimewakutanisha wataalam na wadau mbalimbali wakiwemo watalaam kutoka Mpango wa taifa wqa kudhibiti malaria (NMCP), Shirika la Afya Duniani (WHO),

TPH, Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) Chuo kikuu cha Dar es Salaam, na wataalam kutoka Tanzania Field Epidemiology and Laboratory Training (TFELTP) kwa lengo la kupitia na kuboresha viashiria,

na taratibu za ukusanyaji, uchambuzi na matumizi ya taarifa za malaria. Akizungumza katika kikao hicho, Mratibu wa zoezi hilo, kwa niaba ya Mkuu wa Kitengo cha ufuatiliaji na tathmini wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP),

Pai Chambongo, amesema kuwa maboresho ya mwongozo huo yanalenga kuboresha ili uendane na Mpango mkakati wa kudhibiti na kutokomeza malaria 2026-2030 na kuimarisha ufutailiaji wa wagonjwa wa malaria na kuchukua hautua stahiki pale inapohitajika kwa kuzingatia takwimu za wagonjwa wa malaria nchini,.

kuwa mwongozo huo utakuwa nyenzo muhimu katika kuhakikisha taarifa zinazokusanywa zinakuwa sahihi, za kuaminika na zinatumika kwa wakati katika kufanya maamuzi ya kitaalamu, kupanga mikakati na kutathmini ufanisi wa afua zinazotekelezwa katika mapambano dhidi ya malaria nchini. Mwongozo huu utakapokamilika, utaiwezesha -Wizara ya Afya – Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria na wadau wake kuimarisha uwajibikaji, kufanya maamuzi yanayotegemea ushahidi na kuhakikisha rasilimali za kupambana na malaria zinatumika kwa ufanisi.

utasaidia kupima mchango wa afua mbalimbali katika kupunguza maambukizi na vifo vya malaria, kuelekea malengo ya kudhibiti na hatimaye kutokomeza malaria nchini ifikapo mwaka 2030.

}