Girl in a jacket

MINISTRY OF HEALTH

National Malaria Control Programme (NMCP)

Girl in a jacket

MAFUNZO YA AFUA YA UNYUNYIZIAJI VIUADUDU VYA KIBAIOLOJIA KWA WATAALAM WA AFYA NGAZI YA MKOA NA HALMASHAURI (MIKOA YA MWANZA, SIMIYU NA MARA)

Posted on: January 28th, 2026

Timu ya wataalam wa udhibiti wadudu dhurifu kutoka Wizara ya Afya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) pamoja na wadau kutoka SWISS TPH katika Mradi wa TEMT kwa pamoja wanafanya mafunzo ya unyunyiziaji wa Viuadudu vya Kibailojia kwenye mazalia ya mbu, kwa wataalam wa Afya ngazi ya Halmashauri kutoka katika Mikoa ya Mwanza, Simiyu na Mara. Mafunzo haya ya Siku mbili yanafanyika kuanzia Januari 27 hadi 28, 2026 mkoani Mwanza na yanahusisha elimu ya nadharia na mafunzo kwa vitendo.

Mafunzo kwa vitendo yamefanyikia katika wilaya ya Nyamagana  eneo la Nyanshishi ambapo kuna  mazalia ya Mbu. Wataalam hao wamefundishwa jinsi ya kutambua aina ya viluilui wa mbu, kutambua aina ya  viuadudu vya kibailojia vinavyotumika kuwaangamiaza viluilui hao pamoja na njia rahisi ya kupima  na kufanya makadirio ya ukubwa wa zalia kabla ya kuweka viuadudu hivyo.

Aidha wamefundishwa jinsi ya kupima kiwango cha viuadudu vya kibailojia kinachotakiwa kuwekwa kwenye kila zalia kutokana na ukubwa wa zalia na aina ya viuadudu vya kibailojia vinavyotumika, pamoja na kufanya tathimini na ufuatiliaji wa ufanisi wa viuadudu katika mazalia hayo.

Afua ya unyunyiziaji viuadudu vya kibailojia katika mazalia ya mbu ina umuhimu mkubwa katika mapambano dhidi ya malaria inchini kwa kuwa:

  • Hupunguza idadi ya mbu kabla  hawajawa wapevu ambao nihatari katika kueneza malaria na magonjwa mengine yanayoenezwa na mbu
  • Ni njia endelevu na rafiki kwa mazingira.
  • Inashirikisha jamii kwa mafanikio endelevu na ya muda mrefu
  • Huwajengeaa uwezo wataalam katika kutekeleza mbinu bora za utekelezaji wake na  kuongeza ufanisi wa mapambano dhidi ya mbu waenezao malaria  katika jamii zetu.

Kwa pamoja tunaweza kutokomeza mazalia ya mbu na kulinda afya ya jamii!

 “Ziro malaria inaanza na Mimi, inaanza na wewe inaanza na sisi sote

}