Girl in a jacket

MINISTRY OF HEALTH

National Malaria Control Programme (NMCP)

Girl in a jacket

MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WATENDAJI NGAZI YA MKOA NA HALMASHAURI KUTOKA MIKOA YA ARUSHA, KILIMANJARO NA MANYARA KWA AJILI YA KUTEKELEZA AFUA UNYUNYIZIAJI WA VIUADUDU VYA KIBAIOLOJIA

Posted on: March 13th, 2026

Mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji ngazi ya Mkoa na Halmashauri katika kutekeleza afua ya kuangamiza viluilui vya mbu kwa kutumia viuadudu vya kibaiolojia yameendelea kutolewa kwa Wataalam wa afya kutoka katika mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro. Mafunzo haya yanatolewa na wataalam wa udhibiti wadudu dhurifu kutoka Wizara ya Afya -Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Taasisi ya Afya ya Ifakara - IHI, pamoja na wadau kutoka SWISS - TPH katika Mradi wa TEMT.

Mafunzo haya ya siku mbili yanafanyika mkoani Kilimanjaro katika Manispaa ya Moshi kuanzia tarehe 12 hadi 13 Machi, 2026 na yanahusisha elimu ya nadharia na mafunzo kwa vitendo.

Mafunzo kwa vitendo yamefanyikia katika eneo la Bomambuzi Manispaa ya Moshi ambapo kuna  mazalia ya Mbu. Wataalam hao wamefundishwa jinsi ya kutambua aina ya viluilui wa mbu, kutambua aina ya  viuadudu vya kibailojia vinavyotumika kuwaangamiza viluilui hao pamoja na njia rahisi ya kupima  na kufanya makadirio ya ukubwa wa mazalia kabla ya kuweka viuadudu hivyo.

Aidha, wataalam hao wamefundishwa jinsi ya kupima kiwango cha viuadudu vya kibailojia kinachotakiwa kuwekwa kwenye kila zalia kutokana na ukubwa wa zalia pamoja na kufanya tathimini na ufuatiliaji wa ufanisi wa viuadudu katika mazalia hayo.

Pamoja na kuwepo kwa kiwango cha chini cha maambukizi ya malaria katika mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro, afua ya unyunyiziaji viuadudu vya kibailojia kwenye mazalia ya mbu bado ina umuhimu mkubwa kwa sababu:

  • Inazuia kuongezeka kwa idadi ya mbu wapevu ambao nihatari katika kueneza malaria na magonjwa mengine yanayoenezwa na mbu
  • Inasaidia kufikia malengo ya kutokomeza malaria nchini.
  • Huwajengeaa uwezo wataalam katika kutekeleza mbinu bora za utekelezaji wake na  kuongeza ufanisi wa mapambano dhidi ya mbu waenezao malaria  katika jamii zetu.

Kwa pamoja tunaweza kutokomeza mazalia ya mbu na kulinda afya ya jamii!

 “Ziro malaria inaanza na Mimi, inaanza na wewe inaanza na sisi sote

}