MKURUGENZI WA UTAWALA NA RASILIMALI WATU WIZARA YA AFYA AHIMIZA KUONGEZA JUHUDI KATIKA KUPAMBANA NA UGONJWA WA MALARIA
Posted on: February 26th, 2025
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Wizara ya Afya, Bw. Issa Ng’imba amewahimiza watumishi wa wizara ya Afya katika mpango wa Taifa wa kudhibiti malaria kuongeza juhudi za makusudi za kupambana na ugonjwa wa Malaria nchini. Bwana Ng’imba ameyasema hayo alipokuwa anaongea na watumishi hao katika kikao chao cha kutathimini utendaji wa kazi ili kuongeza tija katika mapambano dhidi ya malaria nchini. Kikao kazi hicho kimefanyikia mkoani Arusha.
“Ni Lazima kujenga umoja (team work) katika utendaji kazi wenu utakaopelekea kufikia malengo mliojiwekea kama Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria ya kuwezesha jamii kuondokana na ugonjwa wa malaria. Kila mtu amuheshimu mwenzake, mfanye kazi kwa kujituma na weledi zaidi kwani kila mtu ana mchango katika mafanikio ya programu.”
Mkurugenzi pia amesisitiza juu ya matumizi mazuri ya rasilimali katika kufanikisha majukumu yetu. Ili kuweza kufikia malengo tuliyojiwekea. Ni muhimu pia kujikita kwenye elimu ya uwekezaji ili kuweza kujiimarisha kiuchumi pamoja na kufuatilia michango yetu kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii ili kujua hali na maendeleo ya michango yetu na kuweka taarifa zetu vizuri.
Maeneo mengine ya kipaumbelle aliyosisitiza ni pamoja na ubinifu katika kuimarisha utendaji kazi wenye ufanisi na tija, ushirikiano na ushirikishwaji na kufanya kazi kwa umoja na upendo ili kuongeza morali na utendaji kazi mzuri kwa watumishi.
Aidha, Mkurugenzi amesisitiza juu ya suala la uwazi na uwajibikaji lizingatiwe na kusisitizwa ili kila mtumishi afahamu wajibu wake na atimize majukumu yake.. Pia utunzaji wa siri na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ikiwemo kutoshiriki suala la rushwa, urasimu uliokithiri, hoja hasi, masuala ya ubaguzi, rushwa, ulevi wa kupindukia
Tukiweza kutekeleza hayo, tutaweza kupata mafanikio katika kufikia malengo ya kutokomeza ugonjwa wa malaria hapa nchini.