Girl in a jacket

MINISTRY OF HEALTH

National Malaria Control Programme (NMCP)

Girl in a jacket

TIMU YA WATAALAM KUTOKA MFUKO WA DUNIA WA KUPAMBANA NA MAGONJWA YA MALARIA, UKIMWI NA KIFUA KIKUU (GFCT) YAKUTANA NA WATAALAM KUTOKA MPANGO WA TAIFA WA KUDHIBITI MALARIA (NMCP) KUJADILI UTEKELEZAJI WA AFUA ZA UDHIBITI WA MALARIA, HALI YA UPATIKANAJI WA BI

Posted on: March 25th, 2026

Timu ya wataalam kutoka Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Magonjwa ya Malaria, UKIMWI na Kifua kikuu leo tarehe 25 Mwezi Machi,2026 imekutana na wataalam kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) pamoja na wadau mbalimbali Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili maendeleo ya utekelezaji wa afua za kudhibiti malaria nchini.

Mkutano huo umejikita katika kutathmini utendaji wa programu, mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zinazoathiri utekelezaji wa afua mbalimbali za kudhibiti ugonjwa huo.

Katika kikao hicho, masuala ya kifedha yamejadiliwa kwa kina yakihusisha hali ya matumizi ya rasilimali fedha (absorption rate) na ufanisi wa matumizi ya fedha za ufadhili.

Timu ya GFCT wamesisitiza umuhimu wa kuhakikisha rasilimali zilizopo zinatumika kwa ufanisi ili kufikia malengo ya kupunguza maambukizi na vifo vitokanavyo na Malaria nchini.

Aidha, mkutano huo umejadili masuala ya usimamizi wa ununuzi na ugavi (PSM), hali ya mnyororo wa ugavi (pipeline), pamoja na maendeleo ya oda za ruzuku ya mwaka 2024 mpaka 2026.

Pia, Timu hizo zilitathmini hatari mbalimbali zinazoweza kuathiri upatikanaji wa bidhaa muhimu za afya na kuweka mikakati madhubuti ya kupunguza athari za hatari hizo katika utekelezaji wa programu.

Kwa upande wake, timu ya NMCP iliwasilisha hali ya ugonjwa wa Malaria nchini, ikionesha mwenendo wa maambukizi katika maeneo mbalimbali pamoja na hatua zinazochukuliwa kudhibiti ugonjwa huo.

Uwasilishaji huo umejumuisha utekelezaji wa Afua muhimu pamoja na hali ya upatikanaji wa dawa za Malaria kwa mwaka 2025, huku wadau wakiahidi kuendelea kushirikiana kuimarisha mapambano dhidi ya malaria nchini.

}