Girl in a jacket

MINISTRY OF HEALTH

National Malaria Control Programme (NMCP)

Girl in a jacket

UKWAA LA MALARIA LAFANYIKA LEO TAREHE 23 APRILI 2026, JIJINI DODOMA, KUELEKEA SIKU YA MALARIA DUNIANI - APRILI 25, 2026.

Posted on: April 23rd, 2026

Kuelekea Siku ya Malaria Duniani, Taasisi ya Afya ya Ifakara (Ifakara Health Insitute) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Wadau, imeendesha jukwaa la Malaria (Malaria forum) lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Royal Village, Jijini Dodoma.


Jukwaa Hilo limewaleta pamoja Viongozi mbalimbali, Watafiti, Wanasayansi, wataalamu wa afya pamoja na Wadau mbalimbali ili kujadili dhamira kuu ya kuendeleza juhudi katika mapambano dhidi ya malaria hapa nchini.

Akifungua jukwaa hilo Dkt. Ahmed Makuwani – Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto – Wizara ya Afya ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe amesisitiza kuwa mapambano dhidi ya malaria yamefikia wakati muhimu kwani mikakati na afua madhubuti za udhibiti wa malaria zinatekelezwa kwa ufanisi hapa nchini. Dkt. Makuwani, ameeleza kuwa maendeleo ya kisayansi, ubunifu pamoja na tafiti mbalimbali zimeleta mageuzi na kuboresha utekelezaji huo kwa lengo la kuelekea kutokomeza ugonjwa wa malaria ifikapo mwaka 2030.

Dkt. Makuwani pia amesisitiza kuwa, pamoja na mafanikio yaliyofikiwa katika mapambano dhidi ya malaria, bado tunatakiwa kuongeza uwekezaji katika mapambano haya na lazima tuchukue hatua sasa kwani bila kuwa na dhamira endelevu, mafanikio ambayo tumeyapata yanaweza kurudi nyuma kwa haraka. Mapambano dhidi ya malaria ni jukumu la kila mtu na uwajibikaji wa pamoja

Siku ya Malaria Duniani inaadhimishwa kila mwaka kila ifikapo tarehe 25 Aprili kwa lengo la kutafakari utekelezaji wa mikakati iliyopangwa ya kudhibiti ugonjwa wa malaria, mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizopo na njia za kukabiliana nazo, ili kufikia lengo la kutokomeza Malaria nchini ifikapo mwaka 2030.

Kauli mbui ya mwaka huu inasema Tumedhamiria Kutokomeza Malaria, Wakati ni sasa, Tunaweza.”. Ziro Malaria inaanza na Mimi.

}