Girl in a jacket

MINISTRY OF HEALTH

National Malaria Control Programme (NMCP)

Girl in a jacket

USHIRIKI WA SEKTA MTAMBUKA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA NCHINI

Posted on: February 4th, 2026

Juhudi za kupambana na ugonjwa wa malaria zinahitaji ushiriki wa sekta mbalimbali ili kuweza kufikia lengo la kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2030. Mapambano dhidi ya malaria si jukumu la sekta ya afya pekee, bali ni ushirikiano wa sekta zote muhimu. Maambukizi ya ugonjwa wa malaria yanachangiwa na visababishi kadhaa njie ya sekta ya afya. Zipo sekta mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingine zinachangia katika mapambano dhidi ya malaria hapa nchini. Sekta hizo ni pamoja na mazingira, maji, miundombinu, nyumba na makazi, elimu, kilimo, madini, sekta binafsi, Asasi za kijamii, Taasisi na Viongozi wa Dini na nyingine nyingi.

Katika kuratibu ushiriki wa sekta Mtambuka katika mapambano dhidi ya malaria, Wizara ya Afya- Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP), iliandaa Mwongozo wa Ushiriki wa Sekta Mtambuka katika udhibiti wa malaria nchini. Mwongozo huu umesaidia katika utekelezaji wa kazi mbalimbali na kuunganisha sekta ya Afya na Sekta nyingine. Mpaka sasa tayari sekta 29 zinashirikiana na Wizara ya Afya. Ili kuboresha ushirikiano huo, Maafisa viungo kutoka katika sekta mtambuka walichaguliwa ili waweze kuratibu mapambano dhidi ya malaria katika sekta husika. Sekta zenye maafisa viungo ni pamoja na Wizara zifuatazo: Ulinzi, Ofisi ya Rais -Mipango na Uwekezaji, Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Kilimo, Fedha, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Mifugo na Uvivu, Ofisi ya Rais Utumishi, Madini, Uchukuzi, Mambo ya ndani, Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Nishati, Viwanda na Biashara, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Sheria na Katiba, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Maliasili, Maji, mambo ya Ndani ya Nchi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Polisi na Tume ya Mipango.


Katika kuendeleza uratibu wa kazi za ushiriki wa Sekta Mtambuka, NMCP kwa kushirikiana na wadau - Swiss TPH katika Mradi wa TEMT, wamefanya kikao kazi Januari  29 - 30, chenye lengo la kupanga namna bora ya kuendeleza kazi za sekta mtambuka ili kuongeza tija zaidi.

}