Girl in a jacket

MINISTRY OF HEALTH

National Malaria Control Programme (NMCP)

Girl in a jacket

WATAALAM WA AFYA NGAZI YA MKOA NA HALMASHAURI KUTOKA MIKOA YA GEITA, KIGOMA NA KAGERA WAPEWA MAFUNZO YA UNYUNYIZIAJI VIUADUDU VYA KIBAIOLOJIA MKOANI GEITA

Posted on: January 23rd, 2026

Wataalam wa uthibiti wadudu dhurifu kutoka Wizara ya Afya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI, Taasisi ya Taifa ya utafiti wa magonjwa ya Binadamu (NIMR) pamoja na wadau kutoka SWISS TPH katika mradi wa TEMT wamefanya mafunzo ya unyunyiziaji wa Viuadudu vya Kibailojia kwenye mazalia ya mbu kwa Wataalam wa Afya ngazi ya Halmashauri kutoka katika Mikoa ya Geita, Kigoma na Kagera. Mafunzo haya ya Siku mbili yamefanyika kuanzia Januari 22 hadi 23, 2026.

Lengo la mafunzo haya ni kuwapa uelewa wa viuadudu vinavyotumika na matumizi ya viuadudu hivyo katika kuangamiza viluilui wa mbu kwenye mazalia ya mbu, kutambua aina ya mazalia na viluilui vya mbu vinavyopatikana katika mazalia hayo, kufanya mahesabu ya kiwango cha viuadudu kinachokubalika kuwekwa kwenye kila aina ya ukubwa wa zalia la mbu, ufuatiliaji na kufanya taathimini ya unyunyiziaji uliofanyika pamoja na kuandaa taarifa za zoezi la unyunyiziaji utakavyokuwa unafanyika katika maeneo yao.

Wataalam wa afya waliopata mafunzo haya ni Mratibu wa malaria mkoa na wilaya, Mratibu wa Elimu  ya Afya kwa Umma wilaya, Mratibu wa udhibiti taka ngumu wa wilaya na Wadhibiti wa wadudu dhurifu (Vector Control officers) wa wilaya. Mafunzo haya yalitolewa kwa njia ya nadhalia na vitendo na nimuendelezo wa mafunzo yaliyozinduliwa mkoani Morogoro Desemba 19, 2025 ambayo yanalenga katika kutoa elimu kwa wataalam hao ili waweze kwenda kufanya mafunzo ya unyunyiziaji viuadudu hivi kwa Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii watakaofanya kazi katika maeneo yao. Aidha washiriki walijifunza kutumia aina tofauti ya viuadudu kutokana na aina ya mazalia na viluilui vya mbu vinavyopatikana katika mazalia hayo.

Afua ya unyunyiziaji wa Viuadudu vya Kibaiolojia  inatekelezwa kwa lengo la kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria nchini ili kufikia lengo la kutokomeza ugonjwa huu  ifikapo mwaka 2030.

}