Girl in a jacket

MINISTRY OF HEALTH

National Malaria Control Programme (NMCP)

Girl in a jacket

WIZARA YA AFYA KUPITIA MPANGO WA TAIFA WA KUDHIBITI MALARIA WAKUTANA NA VIONGOZI WA CONAMET

Posted on: March 9th, 2025

Wizara ya Afya kupitia mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria (NMCP) leo Tarehe 10 Machi, 2025 Jijini Dodoma imekutana na Viongozi wa Mtandao wa Asasi za Kiraia zinazojihusisha na mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria nchini (CONAMET) kwa lengo la kujitambulisha na kupitia maendeleo ya utekelezaji wa shughuli za kijamii za kupambana dhidi ya ugonjwa Malaria.

Kikao hicho ambacho kimeongozwa na Mkuu wa Program Kutoka wizara ya Afya Dkt. Samwel Lazaro kimebainisha maeneo ya ushirikiano baina ya Wizara  na Asasi hizo katika kubaini maeneo yenye changamoto na kupendekeza mikakati ya kuzitatua ili kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria nchini. Akioongea katika kiko hicho Dr. Lazaro amesisitiza kuwa utendaji  wa kazi wa CONAMET unatakiwa kuwa chachu ya utafutaji wa rasilimali fedha nje ya Serikali kwa  ajili ya kuendeleza mapambano dhidi ya malaria nchini.

Pamoja na mambo mengine, mwenyekiti wa CONAMET Tanzania Bw, Gensoko Paul amemuomba  mkuu wa Program  wapate wataalam kutoka  katika Mpango wa Taifa wa kudhibiti ugonjwa wa Malaria (NMCP) ili wawajengee uwezo kuhusiana na afua mbalimbali za malaria zinazotekelezwa kwenye Jamii ili wapate uelewa mzuri kwa ajili ya kuzitekeleza kwa ufanisi

}