Girl in a jacket

MINISTRY OF HEALTH

National Malaria Control Programme (NMCP)

Girl in a jacket

ZOEZI LA KUFANYA MPANGO WA MANUNUZI NA MAHITAJI YA BIDHAA ZA MALARIA

Posted on: February 5th, 2026

Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria upo katika hatua za kukamilisha kuandaa Mpango Mkakati wa mwaka 2026-2030 ambapo afua zote zinazotekelezwa katika kipindi hicho zinatakiwa kuorodheshwa zikiambatana na gharama za kutekeleza afua hizo. Ili kufanikisha hilo Wizara ya Afya imeandaa kikao kazi cha kuanisha mpango wa manunuzi wa mahitaji ya bidhaa za malaria (maoteo) ambapo wataalamu mbalimabali kutoka Wizara ya Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi pamoja na Wadau, wanakutana mkoani Morogoro kuanzia tarehe 02 Februari mpaka tarehe 11 Februari 2026 kwaajili ya kuandaa mpango huo.

Akiongea kwenye uzinduzi wa kikao kazi hicho Ndugu Mayanya Said Mayanja ambaye ni Mratibu wa Maoteo ya bidhaa za afya kutoka Ofisi ya Mfamasia Mkuu wa Serikali - Wizara ya Afya, amesema kua maoteo ya bidhaa za afya nchini yanafanywa kwa mfumo wa “bottom up approach” ambapo mchakato huo huanzia vituo vya huduma za afya na kuwezesha ngazi ya maamuzi (Wizara) kufanya maamuzi kwa kuzingatia mahitaji halisi yaliyo ainishwa na vituo hivyo. 

Katika kufanya maoteo wataalamu wanaangalia matumizi ya mwaka uliopita na kuweka makisio ya matumizi ya mwaka unaofuata ambapo dhana mbalimbali zinaangaliwa ikiwemo dhana ya idadi ya watu (population) ambapo takwimu za idadi ya watu na matarajio yake zinatumika, dhana ya matumizi ya bidhaa yaliyopita (consumption), dhana ya taarifa za ugonjwa (Morbidity), kiwango cha maambukizi, idadi ya wagonjwa pamoja na idadi ya vifo na malengo ya mpango wa kudhibiti malaria (Program Target)

Mpango huu wa manunuzi utasaidia kuweza kupanga mahitaji ya bidhaa za malaria na kuweza kukamilisha maandalizi ya Mpango Mkakati wa Malaria wa mwaka 2026-2030 pamoja na kufanya maombi ya fedha kutoka Mfuko wa Dunia wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kukuu na Malaria (Global Fund) kwa mzunguko wa 8 na kuwezesha jitihada za Serikali katika mapambano ya dhidi ya malaria ili hatimae kuweza kufikia lengo la kutokomeza ugonjwa huu ifikapo mwaka 2030.

}