ZOEZI LA KUPITIA NA KUHUISHA TAARIFA ZA MNYORORO WA UGAVI WA BIDHAA ZA MALARIA LAFANYIKA
Posted on: July 4th, 2026Mororgoro
Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) na Ofisi ya Mfamasia Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) pamoja na wadau, ina jukumu la kufuatilia na kuhakikisha bidhaa za malaria zinapatikana muda wote ili kutoa huduma stahiki kwa walengwa.
Upatikanaji wa bidhaa hizo unatoa uhakika wa utekelezaji wa afua mbalimbali za kudhibiti ugonjwa wa malaria kama ilivyoainishwa katika Mpango Mkakati wa Malaria.
Kwa kufanikisha hili, wataalam kutoka Wizara ya Afya, OWM-TAMISEMI pamoja na wadau wameandaa kikao kazi kinachofanyika mkoani Morogoro kwaajili ya kupitia takwimu za malaria, bidhaa zilizopo na zinazotarajia kuletwa nchini ili kuweka sawa mahitaji ya bidhaa zinazohitajika kwa kuzingatia mahitaji halisi ya sasa.
Taarifa hizo zitatumika katika mipango mbalimbali ikiwemo kuwezesha Serikali pamoja na wadau kutekeleza afua mbalimbali katika kupambana na ugonjwa wa malaria na hatimae kuwezesha jitihada za kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030.