Girl in a jacket

MINISTRY OF HEALTH

National Malaria Control Programme (NMCP)

Girl in a jacket

DAWA ZA ARV, MALARIA NA KIFUA KIKUU ZINATOLEWA BURE; WAZIRI UMMY MWALIMU

Posted on: November 30th, 2022

Na Englibert Kayombo WAF - Kibaha, Pwani.

Serikali kwa kushirikiana na Global Fund bado zinaendela kukabiliana na magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria kwa kuhakikisha matibabu ya magonjwa hayo yanapatikana bure na kwa urahisi katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. ummy Mwalimu akiwa na mgeni wake Bw. Peter Sands Mtendaji Mkuu wa Global Fund walipotembelea Zahanati ya Disunyara iliyopo Wilaya ya Kibaha kuona hali ya utoaji huduma na utekelezaji wa afua za mapambano dhidi ya magonjwa hayo

}