Girl in a jacket

MINISTRY OF HEALTH

National Malaria Control Programme (NMCP)

Girl in a jacket

MAADHIMISHO YA SIKU YA MALARIA DUNIANI NA UZINDUZI WA KAMPENI YA UGAWAJI WA VYANDARUA VYENYE DAWA VYAFANYIKA MKOANI KIGOMA

Posted on: May 5th, 2025

Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani yakiambatana na uzinduzi wa kampeni ya ugawaji wa vyandarua kwa wananchi yamefanyika ngazi ya Mkoa tarehe 26 Aprili 2025 katika kituo cha afya cha Ujiji  Manispaa ya Kigoma.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Mgeni Rasmi Afisa Tawala Wilaya ya Kigoma Bi. Dorah Buzaile kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, pamoja na Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Kigoma.

Akiongea kwenye hafla hiyo Bi Dorah Buzaile kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma alisema  “katika kuadhimisha wiki ya malaria duniani, mkoa wetu leo unazindua kampeni ya ugawaji wa vyandarua ngazi ya kaya kwa wilaya zetu zote 8 za mkoa wa Kigoma. Ugawaji wa vyandarua mkoani kwetu  ni jitihada chanya za Serikali katika kupambana na ugonjwa wa malaria hapa nchini. Hivyo napenda kuwataarifu kuwa, kampeni hii ya Ugawaji wa vyandarua vyenye dawa mkoa wa Kigoma imeanza rasmi tarehe 26/04/2025.”

  Bi Dorah Buzaile alisema kuwa katika kampeni hiyo Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais -TAMISEMI, Bohari ya Dawa (MSD) na wadau wake watagawa vyandarua takribani 1,414,251 kwa Mkoa wa Kigoma na alisisitiza kuwa kila mwananchi aliejiandikisha ahakikishe anakwenda na kuponi yake katika eneo alilopangiwa kupokelea chandarua chake ili apatiwe chandarua  na ahakikishe anakitumia kwa ajili ya kujikinga na mbu ili kuepuka maambukizi ya Malaria na sio matumizi mengine kama vile kufugia kuku, kuvulia samaki au matumizi mengine yasiofaa.

}