Girl in a jacket

MINISTRY OF HEALTH

National Malaria Control Programme (NMCP)

Girl in a jacket

MAFUNZO YA UDHIBITI WA MBU KWA KUTUMIA VIUADUDU VYA KIBAIOLOJIA NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA KWA WAKUFUNZI, YAZINDULIWA- MOROGORO

Posted on: December 22nd, 2025

Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI pamoja na wadau wa maendeleo inatekeleza afua mbalimbali za kupambana na malaria ikiwemo afua ya udhibiti mbu kupitia unyunyuziaji wa viuadudu vya kibaiolojia na udhibiti wa mazingira.

Katika kutekeleza afua hii, Wizara imezindua mafunzo kwa Wakufunzi juu ya udhibiti wa mbu kwa kutumia viuadudu vya Kibaiolojia na udhibiti wa mazingira. Uzinduzi huo umefanyika tarehe 19 Desemba, 2025 Mkoani Morogoro, ambapo jumla ya washiriki 103 kutoka katika Halmashauri 27 za mikoa ya Morogoro, Pwani na Tanga walipatiwa mafunzo kwa njia ya nadharia na vitendo.


Wakufunzi hao ni waratibu wa malaria kutoka katika ngazi ya Halmashauri na Mkoa, Waratibu wa udhibiti wadudu dhurifu (vector control coordinator), Maafisa mazingira pamoja na waratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma.

Mafunzo hayo yalizinduliwa na mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii kutoka katika OWM-TAMISEMi Bi. Stella Kajange. Akiwasilisha hotuba ya ufunguzi, Bi. Stella Kajange  alisema kua Serikali imedhamiria kupambana na ugonjwa wa Malaria na kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imetenga kiasi cha Shilingi za Kitanzania Bilioni 10 kwa ajili ya kununua viuadudu vya Kibaiolojia vinavyozalishwa hapa nchini kutoka katika kiwanda cha Tanzania Biotech Products Ltd kilichopo Kibaha Mkoani Pwani na kwa ajili ya Halmashuri zote 184 kuvichukua viuadudu kutoka kwenye kiwanda hicho na kuvitumia kulingana na miongozo iliyopo.

Aidha, Bi Stella alisistiza kuwa, ni muhimu  kwa wataalamu kuzingatia mafunzo hayo ili kusaidia kuongeza ujuzi na ufanisi katika kudhibiti mbu na kupambana na ugonjwa wa malaria. Wakufunzi hao pia walisisitizwa kusimamia utekelezaji wa afua za udhibiti wa mbu na usimamizi wa sheria ya afya ya jamii ya mwaka 2009 pamoja na sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 na kuhakikisha kila Halmashauri inatenga fedha kwaajili ya utekelezaji wa shughuli za malaria ili kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria.

}