MIFUMO YA AFYA ISOMANE ILI KURAHISISHA UPATIKANAJI WA HUDUMA KWA WANANCHI
Posted on: August 18th, 2024Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema mifumo ya huduma za matibabu kwa wagonjwa inatakiwa isomane kuanzia kwenye Zahanati hadi Hospitali za Rufaa ili kurahisisha huduma hizo kupatikana kwa urahisi na ufanisi kuwafikia wanannchi.
Waziri Mhagama amesema hayo leo Agosti 16, 2024 katika Ofisi ya Wizara Afya mji wa Serikali, Mtumba mkoani Dodoma wakati akizungumza na Menejimenti pamoja na watumishi wa Sekta ya Afya baada ya kukabidhiwa ofisi rasmi.
"Tunawenzetu ambao wana simamia Afya msingi na wengine tunaendelea huku juu lakini Mtanzania anaetibiwa kwenye Afya msingi na huku juu ni huyohuyo mmoja, tufikie mahali mgonjwa akitibiwa kwenye Zahanati mganga wa Hospitali ya Wilaya awe anajua kuwa kuna mgonjwa anatibiwa kwenye Zahanati lakini kwa ugonjwa huo hawezi kupata huduma hiyo kwenye Zahanati." Ameeleza Mhe. Mhagama