Girl in a jacket

MINISTRY OF HEALTH

National Malaria Control Programme (NMCP)

Girl in a jacket

MKURUGENZI MSAIDIZI WA UTAWALA WIZARA YA AFYA AKUTANA NA WATUMISHI WA MPANGO WA TAIFA WA KUDHIBITI MALARIA KUJADILI MASUALA MBALIMBALI YA KUBORESHA UTENDAJI KAZI

Posted on: September 30th, 2025

Watumishi wa mpango wa taifa wa kudhibiti malaria wizara ya afya, wamekutana na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu kuboresha utendaji wao wa kazi kilichofanyika tarehe 30 septemba, 2025. Katika kikao hicho vitengo vyote vya mpango wa taifa wa kudhibiti malaria viliwasilisha utekelezaji wao wa kazi.

Katika kikao hicho, mkurugenzi msaidizi wa utawala ndugu dany temba amewasihi watumishi wa wizara ya afya katika mpango wa taifa wa kudhibiti malaria kuwajengea uwezo watumishi waliopo chini yao ili kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yao. Bwana Temba aliongeza kuwa watumishi wa umma tunatakiwa kusaidiana na kushirikiana kwenye masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya kikazi na masuala ya kijamii. Aidha bwana Temba aliwakumbusha watumishi hao kufuatilia masuala yao ya kiutumishi mapema kuliko kusubiria wakati mtumishi anapokaribia  kustaafu utumishi wa umma.

Naye kaimu meneja wa mpango wa taifa wa kudhibiti malaria, bi Anna David amesistiza kuwa ni muhimu kila mwezi kufanyika kwa kikao kazi ili kujadili hali ya utendaji kazi wa programu kwa kila mwezi na kuweka mipango mikakati kwa mwezi unaofuata. “ni muhimu kila kitengo kutoa mrejesho wa nini kimefanyika kwenye kikao na mpango wa mwezi unaofuata. Bi Anna aliongeza vikao hivi vina umuhimu katika kuongeza ufanisi wa kazi na kusistiza watumishi wote wawe wanahudhuria vikao hivyo

}