MPANGO WA TAIFA WA KUDHIBITI MAARIA WAFANYA WAFANYA MKUTANO NA TIMU YA OIG KUKAGUA UTEKEEZAJI NA MAPITIO YA BUDGET YA UFADHII WA GOBA FUND - DODOMA
Posted on: November 30th, 2025Mpango wa Taifa wa Kudhibiti malaria, leo tarehe 1 Disemba, 2025, umekutana na timu ya wataalam wakaguzi kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Kifua Kikuu, UKIMWI na Malaria (Office of the Inspector General – OIG), katika ofisi za Mpango huo zilizopo Mtumba, jijini Dodoma. Lengo la mkutano huu ni kufanya zoezi la ukaguzi wa kazi za malaria zinazotekelezwa kupitia ufadhili wa Global Fund hususani kupitia na kukagua mchakato wa mapitio ya bajeti yaliyofanyika mara baada ya mabadiliko ya sera za kimataifa katika ufadhili wa kazi za Global Fund ambayo yalipelekea kupunguza kwa baadhi ya kazi na fedha katika bajeti husika.