Girl in a jacket

MINISTRY OF HEALTH

National Malaria Control Programme (NMCP)

Girl in a jacket

WAJUMBE WA BARAZA LA KUTOKOMEZA UGONJWA WA MALARIA NCHINI WAKUTANA.

Posted on: September 30th, 2025

Wajumbe wa baraza la kutokomeza ugonjwa wa malaria Tanzania (EMCT) wamekutana Jijini Dar es Salaam na kujadili hoja mbalimbali za utekelezaji wa mikakati ya kupambana na Malaria. Vilevile viongozi wa dini ambao ni wajumbe wa baraza hilo wamejadili namna sahihi ya kuhusisha taasisi za dini katika mapambano ya ugonjwa wa malaria ili kuweza kufanya uhamasishaji na uelimishaji juu ya ugonjwa wa malaria na kuweza kufikia lengo la kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2030.

Akizungumza kwenye kikao hicho, mwenyekiti wa Baraza hilo Mh. Leodigar Tenga amewashukuru viongozi wa dini kwa namna wanavyojitoa kuelimisha na kuhasamasisha jamii juu ya mapambano ya ugonjwa wa malaria na amewasisitiza wajumbe wa kikao kuwa, baraza linatakiwa kujikita kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kuendelea kutekeleza afua za kudhibiti ugonjwa wa malaria nchini ili tufikie lengo la Ziro Malaria ifikapo mwaka 2030. Bwana Tenga aliwaeleza wajumbe hao kuwa waendelee kushawishi watu wenye utayari wa kuchangia baraza katika maeneo yao ili kupata fedha zitakazowezesha utekelezaji wa afua zinazotakiwa kutekelezwa kwa ajili ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria.

Naye kaimu mkuu wa program kutoka Wizara ya Afya Dkt. Samwel Lazaro amewaeleza wajumbe hao kuwa wizara itaendelea kushirikiana na baraza la kutokomeza malaria na kuhakikisha tunaweka mikakati mizuri ikiwemo kuwajengea uwezo viongozi wa dini ya kuweza kuleta tija katika kupambana na malaria

}