WATAALAM WA AFYA NA ELIMU KUTOKA HALMASHAURI ZA MIKOA YA PWANI, DAR ES SALAAM, TANGA NA MOROGORO WAPEWA MAFUNZO YA ZOEZI LA UTAFITI WA UGONJWA WA MALARIA NA HALI YA LISHE KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MISINGI
Posted on: October 15th, 2025Zoezi la utafiti wa ugonjwa wa malaria kwa wanafunzi wa shule za Msingi za umma, na watoto chini ya umri wa miaka mitano (Miezi 6 – 59) linategemewa kuanza rasimi nchini mnamo mwezi Novemba, 2025. Zoezi hili litaenda sambamba na upimaji wa hali ya lishe kwa wanafunzi wa shule za msingi za umma.
Akizungumza kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam juu ya zoezi hilo, Mratibu wa utafiti huo kutoka Wizara ya Afya – Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Ndugu Frank Chacky alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa kwa waratibu na wasimamizi wa zoezi hili ili kuleta ufanisi mzuri wakati wa utekelezaji wake katika ngazi ya mikoa na Halmashauri. Aidha, Ndugu Chacky aliongeza kuwa utafiti huu utasaidia kujua hali ya maambukizi ya malaria kwa wanafunzi wa shule za misingi, hali ya lishe pamoja na kutambua sababu zinazopelekea hali hizo kwa wanafunzi wa shule za misingi nchini Tanzania ili hatua Madhubuti zichukuliwe.
Wataalamu waliojengewa uwezo ni Waratibu wa Malaria wa Mikoa na Halmashauri,Maafisa Elimu wa shule za misingi na Wauguzi pamoja na waratibu wa maabara wa mikao hiyo. Wataalam hao walipitishwa kwenye fomu mbalimbali za kukusanyia taarifa wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo na kuzifanyia mazoezi ya kukusanya taarifa hizo kwenye jamii ambapo pia walipata muda wa kuzifanyia maboresho Wataalam hao waligawiwa vitendea kazi vyao kwa kila Halmashauri kwa ajili ya kwenda kutumia wakati wa kutekeleza zoezi hili katika maeneo yao.
Mafunzo haya yalitanguliwa na mafunzo yaliyofanyika mkoani Njombe kuanzia tarehe 7 – 9 mwezi Oktoba kwa waratibu wa kanda ya kusini na yataendelea kwa waratibu wa kanda ya kati na kaskazini kati ya tarehe 16 – 18 mwezi Oktoba, 2025 na kuhitimishwa kati ya tarehe 20 – 22 mwezi wa 10, 2025 wataalam wa kanda ya ziwa na mikoa ya magharibi mwa Tanzania