Girl in a jacket

MINISTRY OF HEALTH

National Malaria Control Programme (NMCP)

Girl in a jacket

ZOEZI LA UFUATILIAJI NA UHAKIKI WA AFUA YA UELIMISHAJI NA UHAMASISHAJI JAMII JUU YA UDHIBITI WA MALARIA KATIKA MIKOA YA ARUSHA KILIMANJARO, SINGIDA NA KAGERA LAFANYIKA

Posted on: July 3rd, 2026

Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP), kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OW-TAMISEMI), imefafanya zoezi la ufuatiliaji na uhakiki wa utekelezaji wa kazi za uhamasishaji na uelimishaji jamii juu ya ugonjwa wa malaria katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Singida na Kagera.

Zoezi  hili limejumuisha Halmashauri 8 (mbili katika kila mkoa) na kuwezesha jumla ya kata 16 na kaya 80 kutembelewa. Mambo makuu yaliyofanyika katika zoezi hilo ni kufanya tathimini ya uelewa wa wanajamii juu ya ugonjwa wa malaria hususani namna  na mbinu za kujikinga na ugonjwa huo, umuhimu wa  kuchukua hatua stahiki za kimatibabu pindi wanapoona au kuhisi dalili za malaria ikiwemo kuwahi katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kufanyiwa uchunguzi, kupata tiba sahihi na kukamilisha dozi.

Zoezi hili pia limeangalia hali ya umiliki na matumizi sahihi ya vyandarua vyenye dawa kwa wanajamii ili kuweza kujikinga na ugonjwa wa malaria na kuhakikisha jamii inakua salama na yenye afya.

Aidha, katika  zoezi hili, kupitia kwa wanakaya waliotembelewa, imeonekena kuwa wanajamii wanaendelea kupata elimu juu ya udhibiti wa malaria kupitia njia mbalimbali, na pia wanakaya hao wametoa maoni ya kuendeleza hamasa na elimu zaidi ili kuweza kuendelea kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria hapa nchini.

Elimu na hamasa juu ya ugonjwa wa malaria ni muhimu sana ili kuwawezesha wanajamii kuendelea kutumia afua zote muhimu za udhibiti wa malaria zinazotekelezwa hapa nchini. Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendelea kuhakikisha elimu na hamasa ya ugonjwa wa malaria inaendelea kuimarishwa ili kuweza kuchangia katika kufikia lengo la kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2030. 

  “Ziro Malaria Inaanza na Mimi, Inaanza na Wewe, Inaanza na Sisi sote”

}